Kufuatia ajali mbaya
iliyohusisha magari
matatu wilayani Butiama
mkoani Mara idadi ya
watu waliopoteza maisha
ni 38 hadi sasa huku
majeruhi wakiwa ni 80.
Kwa mujibu wa mkuu wa
wilaya ya Butiama
ambaye ni mwenyekiti wa
kamati ya ulinzi na
usalama wilaya hiyo
Anjelina Mabula
aliyezungumza na TBC
muda mfupi uliopita
amesema ajali hiyo
imehusisha basi la AM
Coach lenye namba za
usajili T736 AWJ likitoka
Musoma kwenda Mwanza
limegongana uso kwa uso
na basi T677 CYC J4
Express likitoka Mwanza
kwenda Tarime na gari
jingine dogo aina ya
Nissan Corola P332 KKT
likitoka eneo la Sabasaba
yote yalikutana kwenye
mteremko yakitokea juu
kwenda Darajani katika
kupishana ,kutokana na
spidi waliyokuwa nayo
hawakuweza kupishana
yakagongana na wakati
huo gari dogo likapaki
pembeni nalo likagongwa
kwa nyuma likasukumwa
na kutumbukia mtoni.
Katika gari dogo watu
wawili wamefariki dunia
na majeruhi 36 kutoka
kwenye mabasi nao
wamefariki na majeruhi
80 wamekimbizwa katika
hospitali ya mkoa wa
Mara.
Madereva wote
wamefariki dunia,na
kwamba mizigo ya
majeruhi iko chini ya
ulinzi wa polisi
Post a Comment