Nyumba hiyo ikiwa
imeteketea kabisa. Nyuma
inayomilikiwa na
mfanyabiashara maarufu
mjini Zanzibar, Noushad
Mohammed Suleiman,
iliyopo mtaa wa Kwa Kisasi
barabara ya Bububu,
imeteketea kwa moto.
Nyumba hiyo yenye
vyumba vitatu na msikiti,
iliungua jana jioni kutokana
na hitilafu ya umeme.
Mfanyabiashara Noushad
Mohamed Suleiman
akizungumza na waandishi
wa habari kuhusiana na
tukio la kuungua nyumba
yake. Moto huo umeathiri
vibaya nyumba hiyo,
pamoja na samani zote
zilizomo ndani.
Akizungumza na waandishi
wa habari hizi, mmiliki wa
nyumba hiyo alisema,
chanzo cha moto huo ni
hitilafu ya umeme, ambao
ulianzia katika chumba cha
kushonea na baadae
kuenea sehemu nyengine.
Vitu vingine vilivyoungua ni
nyaraka muhimu, hati za
kusafiria za watoto wake,
televisheni seti sita, friji
mbili, kuka, viyoyozi sita na
samani za vyumba vyote na
kumbi. Alisema thamani ya
vitu vilivyoungua bado
haijajulikana.
Gari za vikosi vya
zimamoto zikiwa katika
eneo la tukio. Hata hivyo,
alikishukuru Kikosi cha
Zima Moto na Uokozi (KZU)
pamojana wananchi kwa
ushirikiano wao
uliofanikisha kuudhibiti
moto huo. Noushad ambae
ni mfanyabiashara
mkubwa, alisema ingawa
nyumba hiyo haijakatiwa
bima, hana wasi wasi na
kwamba katika kipindi
kifupi atajenga tena
nyumba hiyo. Naye Mkuu
wa Kikosi cha Zimamoto
mkoa wa mjini, Ame Ali
Suleiman, alisema walipata
taarifa ya moto huo kupitia
simu ya mkononi majira ya
saa 10:07 za jioni na
walifanikiwa eneo la tukio
saa 10:17.
Vikosi vya zimamoto vya
ZKU vikijitahidi kupambana
na moto huo. Alisema
waliudhibiti moto huo
uliokuwa ukiwana kwa kasi
kutokana na upepo mkali
uliokuwa ukivuma.
Akizungumzia changamoto
walizokumbana nazo
wakati wa uzimaji moto
huo, alisema hawakuwa na
maji ya kutosha hali
iliyowalazimu kurudi tena
mjini kufuata maji.
Kamanda wa Polisi Mkoa
wa mjini magharibi Unguja,
Mkadam Khamis Mkadam,
alisema hakuna mtu
alieathirika na moto huo
wala hakukua na uhalifu
wa aina yoyote
ulioripotiwa. Aliwataka
wanachi kuwa na tahadhari
wanapotumia vitu vya
umeme, pamoja na
kuhakikisha wanazima vitu
vyote wanapomaliza
kutumia.
Post a Comment