Kuanzia siku tatu
zilizopita stori kubwa
kwenye kiwanda cha
burudani Tanzania
imehusu fujo zilizotokea
Ujerumani kwenye show
aliyokwenda kufanya
Diamond Platnumz huko
Stuttgart.
Kilichotokea ni kwamba
saa kumi alfajiri ndio
promota alimpeleka
Diamond kwenye ukumbi
kunakofanyika show. Kwa
nini ilitokea
akamchelewesha? nini
kilitokea baadae? hizi
hapa chini ni kauli za
Diamond mwenyewe
kwenye exclusive na
Clouds fm
1. ‘Mpaka sasa hivi
nashindwa kuelewa tatizo
lilikua nini, siamini
kama
tatizo lilikua ni hela,
balance iliyokua imebaki
ni balance ndogo kama
EURO 3500 hivi ambazo ni
zaidi ya milioni 7 za
Tanzania, ninavyojua
Mapromoter wengi wa nje
wakifanya show huwa
wanauza na vinywaji
wenyewe na wanapata
hela nyingi sana kwenye
vinywaji kuliko hata
viingilio so nahisi labda
walivuta muda ili
waendelee kuuza
vinywaji zaidi’
2. ‘Walichelewa
kunipeleka kwenye show,
walinifata kwenye mida
ya saa tisa usiku na
wakawa hawana hela
yangu iliyobaki,
nikawaambia siendi
kokote mpaka wamalize
kunilipa, walikua na
EURO 1500 wakati nilikua
nawadai 3500
nikawaambia lazima
wanipe hela yote,
wakaifata ndio tukaenda
kwenye show’
3. ‘Tukafika kwenye show
saa10 kasoro, kweli hata
ningekua mimi shabiki
ningekasirika ningefanya
vurugu, wengine walilipa
zaidi ya laki moja na
wametoka kwenye miji na
nchi jirani, niliwaambia
wanipeleke nikafanye
show ndani ya ukumbi
japo tulikuta watu wengi
sana nje lakini
Mapromota walikua
waogawaoga kunipeleka
ndani’
4. ‘Nikakuta watu wengi
na vurugu nje,
nikamwambia promota
atupeleke ndani
tungefika kwenye stage
ingetulia baada ya sisi
kuimba manake ni vitu
tunakutana navyo
kwenye muziki lakini
promota walikua
waogawaoga, askari wa
Ujerumani karibu gari 7
wakaja pale lakini mtiti
ukawa mkubwa’
5. ‘So dakika ya mwisho
tukaona hapashukiki
ndio wakaturudisha
hotelini, kiukweli
nimesikitishwa sana
manake nilikua
nimejipanga vizuri na
ilikua ni mara yangu ya
kwenda kuperform pale
Stuttgart, imenisikitisha
manake watu walikua
kuniona alafu mwisho
ikashindikana
kuwafikishia
walichokitarajia’
6. ‘Nafikiri October
tutakua na show nyingine
na itafanyika kulekule,
nilikua nazungumza na
uongozi wangu kwamba
wanataka show nyingine
na tayari wameshatuma
hiyo hela ya show
nyingine’.
Post a Comment